Soundcloud

Watu 11 wameuawa baada ya makanisa matatu kushambuliwa


Leo May 13, 2018 Washambuliaji wa kujitoa mhanga wamevamia makanisa matatu tofauti nchini Indonesia, katika mji wa pili kwa ukubwa Surabaya na kuua watu takribani 11.
Watu wengine 40 wamejeruhiwa katika mashambulio hayo yaliyotokea kwa kupishana dakika moja kwa kila shambulio. Hakuna kundi lililojitokeza na kudai kuhusika na mashambulio hayo hadi sasa.
Picha za televisheni zinaonesha namna mabaki yalivyotawanywa na shambulio hilo katika moja ya kanisa.
Indonesia, nchi yenye idadi kubwa ya waislamu imekuwa ikikabiliwa zaidi na matukio kutoka kwa wanamgambo wa kiislam katika miezi ya hivi karibuni.

Post a Comment