Soundcloud

Siku 6 baada ya kifo cha Mac Miller haya ndio maneno ya Ariana Grande


Ni takribani wiki moja imepita tokea industry ya Hip Hop Marekani impoteze Rapper Mac Miller kutokana na matumizi ya dawa za kulevya, Ariana Grande ambaye aliwahi kuwa mapenzini na rapper huyo amevunja ukimya na kumuandikia ujumbe.
Ariana Grande hakuandika chochote kuhusiana na kifo cha Mac Miller kwa siku sita zaidi ya kupost picha ya Marehemu Mac Miller bila caption, hivyo kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika ujumbe na kusema kuwa anasikitika kuwa alishindwa kumuondolea maumivu aliyokuwa nayo.

“Nilikukubali tokea siku ya kwanza nakutana na wewe nikiwa na miaka 19 na siku zote nitaendelea kukubali, siamini haupo nasi tena siwezi kufuta hii hali kichwani kwangu, tumekuwa tukizungumza kuhusiana na hili mara nyingi sana, inanichanganya sana na inanihuzunisha sana na sijui nini cha kufanya”
‘Ulikuwa ni rafiki yangu mpendwa kwa muda mrefu zaidi ya chochote kile cha ziada, nasikitika nisingeweza kukutibu au kukuondolea maumivu yako uliyokuwa nayo ila nilipenda kufanya hivyo, ukarimu, roho nzuri hukustahili kupata hayo mapepo, Natumaini upo sawa sasa, Pumzika”

Post a Comment